Terms and Conditions

Katika ununuzi wa mtandaoni, ni muhimu kuelewa masharti na vigezo pamoja na sera ya faragha (privacy policy) ili kuhakikisha kwamba unalinda taarifa zako binafsi na unapata huduma bora. Hapa chini ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia:

Masharti na Vigezo vya kununua bidhaa Online (Online Shopping)

Sheria na Kanuni: Hii ni sehemu inayoeleza sheria zinazotumika kwenye ununuzi wa mtandaoni, kama vile sheria za kulinda watumiaji na sheria za kibiashara.

  1. Mchakato wa Malipo:

Kwa waliopo Mwanza, Geita, dodoma na dar es salaam unalipia baada ya kuwa umeona mzigo.

Utaratibu wa malipo kwa walioko mikoani unalipia kwanza kupitia lipa namba za ofisini baada ya kuwa umefanya malipo na yamepokelewa utatumiwa mzigo wako haraka iwezekanavyo.

 

Unaweza kulipia kupitia lipa namba ya Vodacom, airtel, tigo au halotel, lipa namba zinapatikana kwenye website yetu na jina ni small gifts low price headquarter.

  1. Muda wa kupokea mzigo: Kama umeweka oda ya bidhaa, kwa bidhaa zinazokuja kwa usafiri wa ndege ni kuanzia siku 5 hadi 25 unakuwa umepokea mzigo wako, kwa bidhaa zinazokuja kwa meli ni kuanzia siku 45 hadi 90

Sera ya Faragha (Privacy Policy)

  1. Taarifa Zinazokusanywa: Taarifa zote za binafsi zinazokusanywa kutoka kwa watumiaji, kama vile majina, anwani za barua pepe, taarifa za malipo, na maelezo mengine ya kibinafsi zitatumika kwa lengo maalum tu la kununua bidhaa.

 

  1. Matumizi ya Taarifa: Pia tunaweza kutumia taarifa za mteja kuwasiliana na makampuni ya simu kuulizia kama mteja alifanya malipo (muamala) kwa ajili ya kununua bidhaa, pia kuangalia kama ulipiga simu ofisini na kuweka oda, pia taarifa zako zinaweza kutumika kama vile kutoa huduma, au kwa matumizi ya utafiti wa soko.

 

  1. Ushiriki wa Taarifa: Pia taarifa za mteja zitatumika kuwasiliana na makampuni ya simu kuulizia kama mteja alifanya malipo (muamala) kwa ajili ya kununua bidhaa.

 

  1. Usalama wa Taarifa: Taarifa zako hazitasambazwa wala kutumika tofauti na maelezo yalivyo elezwa katika sera hii.
  2. Haki za Watumiaji: Watumiaji wa huduma zetu ni watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea.
  3. Mabadiliko ya Sera: Kwa mabadiliko ya sere, utatumiwa taarifa siku 30 kabla ya sera mpya kuaza kutumika.
  4. Maelezo ya Mawasiliano: Kwa mawasiliano zaidi, maswali au malalamiko kuhusu sera ya faragha au matumizi ya taarifa zako unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba za simu I will send contacts

Ni vyema kusoma kwa makini masharti na vigezo pamoja na sera ya faragha kabla ya kufanya ununuzi mtandaoni ili kuhakikisha unafahamu haki zako na majukumu yako. Hii itakusaidia kuepuka matatizo na kuhakikisha kuwa unapata huduma bora na salama.

 

MASWALI YALIYO ULIZWA ZAIDI

Small Gifts ni duka la mtandaoni ambalo linauza bidhaa zake mtandaoni na mteja anaweza kununua bidhaa akiwa popote hii inasaidia kuokoa muda na mizunguko isiyokuwa ya lazima.

Small Gifts tunapatikana Dar es salaam, Mwanza, Dodoma na Geita lakini kwa wateja wa mikoani tunawatuma mizigo nauli ni gharama za mteja mwenyewe, Makao makuu ni kanda ya ziwa.

Kwa waliopo Mwanza, Geita, na dar es salaam unalipia baada ya kuwa umepata mzigo,
Utaratibu wa malipo kwa wa mikoani unalipia kwanza kupitia lipa namba za ofisini baada ya kuwa umefanya malipo na yamepokelewa utatumiwa mzigo wako ndani ya siku moja hadi mbili.

Small Gifts imesajiliwa na inatambulika kisheria, tumefuata sheria za kibiashara pia unaweza ukatazama vyeti vya usajili kwenye website yetu.

Muda wa kufika bidhaa inategemea na bidhaa uliyo agiza inaweza kuchukua siku 45-90 kwa bidhaa ndogo ni siku 5-25

Piga namba hizi kwa msaada zaidi 0783888077 Au kama unahitaji kuulizia bidhaa usisite kuwasiliana nasi tunapatikana Kanda ya ziwa, Dar es salaam na Dodoma,
Ahsante na Karibu small Gifts.

LIPA NAMBA

Sasa unaweza kufanya malipo ya bidhaa kupitia lipa namba zilizopo hapo chini.

 

Shopping cart
Start typing to see products you are looking for.